Meek Mill akiwa anakaribia kuachia album, ameanza kuachia vipande cha filamu fupi kusindikiza album yake ya tatu ya Wins and Losses.
Wins And Losses The Movie: Chapter 1
Kipande cha kwanza cha filamu hio fupi inamuonesha msichana akiwa hospitalini anajifungua kwa nguvu, huku baba wa mtoto huyo akiangalia bila uwezo wa kusaidia akiwa na jeraha la risasi pembeni ya kichwa chake.
Meek Mill anaonekana akiimba mistari kadha "Trump aint feeling us, cops still killing us/n---as taking shots cant stop me, they aint real enough," anachana rapa kutoka Philly
Meek pia anamuongelea Ex wake Nicki Minaj katika verse yake."Cut her off, act like she dead and its killing her," anachana Meek Mill.
Wins and Losses imepangwa kutoka Ijumaa ya (July 21), Meek Mill akiwa ameungana na TIDAL kuwezesha baadhi ya show zake zilizopangwa. Kwanza ataanza New York City (July 21), akifatiwa na show katika mji aliotokea huko Philadelphia siku ya (July 24). Na kumalizia tour yake ya miji mitatu kwa kuangusha show Washington D.C siku ya (July 26)
Meek ameanza kuachia baadhi ya nyimbo kutoka album yake ya Tatu.
Mwezi June aliachia "Whatever You Need" aliomshirikisha Chris Brown na Ty Dolla $ign,
Kisha kuachia Y.B.A aliomshirikisha The Dream.
Wiki iliopita alirudi na video yake ya "Issues"
UPDATES
Unaweza kuangalia kipande cha Wins And Losses The Movie: Chapter 2 chini
kipande cha pili kimepewa jina la Wins And Losses - The Trap ikitofautishwa na kipande cha kwanza ambacho alihusisha sana chumba cha hospitali
"The Trap inatupeleka mitaani.
"The Trap inatupeleka mitaani.
UPDATES
Kupitia mtandao wa Youtube, Meek Mill ameachia Kipande cha tatu cha filamu fupi hio
Unaweza kuitazama chini
Mpaka sasa bado haijaeleweka muendelezo endelea kutembelea BLOG YA VIJANA utakuta muendelezo
0 comments :
Post a Comment