.

.

SHOP HERE

News
Loading...

.

.

.

shop now

Kiingilio Mtani Jembe buku tano tu

 
MWAMUZI Ramadhan Ibada ‘Kibo’ kutoka Zanzibar ndiye atasimama katikati kuzichezesha Simba na Yanga katika mechi ya Nani Mtani Jembe itakayochezwa keshokutwa Jumamosi na kiingilio cha chini kimetajwa kuwa Sh 5000 tu.
Kaimu Katibu Mkuu wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Boniface Wambura, ameliambia Mwanaspoti kuwa, Kibo, atasaidiwa na Ferdinand Chacha wa Bukoba na Simon Charles kutoka Dodoma huku mwamuzi wa akiba akiwa Israel Nkongo wa Dar es Salaam.
Wambura alisema mtathimini wa waamuzi katika mchezo huo utakaochezwa Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaamm ni Soud Abdi kutoka Arusha.
Kuhusu viingilio, alisema tiketi zitaanza kuuzwa kesho Ijumaa na kiingilio cha Sh5,000 ni kwa viti vya rangi ya kijani ambavyo vipo 19,648.
Kwa upande wa viti vya rangi ya bluu, alisema kiingilio ni Sh7,000, viti vya rangi ya chungwa ni Sh10,000, VIP C ni Sh15,000, VIP B ni Sh20,000 na VIP A yenye viti 748 tu tiketi moja itapatikana kwa Sh40,000.
Wambura alisema tiketi hizo zitauzwa katika vituo vilivyopo jijini Dar es Salaam ambavyo ni Shule ya Sekondari Benjamin Mkapa, Sokoni Kariakoo, Mgahawa wa Steers ulioko mtaa wa Ohio/Samora, Oilcom Ubungo, Kituo cha Mafuta Buguruni, Dar Live Mbagala, Uwanja wa Uhuru na BMM Salon iliyoko Sinza Madukani.
Wakati huohuo, kikosi cha wachezaji 20 na viongozi tisa cha timu ya taifa ya wanawake chini ya miaka 20 ‘Tanzanite’ kiliwasili jana Jumatano jijini Johannesburg, Afrika Kusini, tayari kwa mechi ya marudiano ya kufuzu Kombe la Dunia la soka la wanawake wa umri huo.
Mechi hiyo itachezwa keshokutwa Jumamosi kwenye Uwanja wa Dobsonville ulioko Soweto, Johannesburg kuanzia saa 9:30 alasiri kwa saa za Afrika Kusini sawa na saa 10:30 jioni kwa saa za Afrika Mashariki.
Share on Google Plus

About feisal pinto

Computer Application Student, Author, Short Stories Writer, Business Proposal Writer, Presenter and Application Builder. Email feisalpinto4@gmail.com for complains and business only.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment

ad