Beki wa Fc Barcelona Carles Puyol anafikiria kustaafu kucheza soka baada ya kushindwa kumudu kucheza katika kinachohitajika kufuatia kukaa nje kwa muda mrefu akiuguza majeraha tofauti.
Puyol ambaye ameichezea Barcelona kwa zaidi ya miaka 15 akiwa nahodha wa timu hiyo amerejea uwanjani wiki chache zilizopita akiwa ametoka kufanyiwa upasuaji wa goti lakini ameshindwa kurejea kwenye kiwango chake cha juu katika baadhi ya mechi alizopewa nafasi ya kucheza.
Kwa sasa Barcelona wanajiandaa kusajili beki mwingine wakati wa dirisha dogo la usajili mwezi januari ili kuziba pengo la Carles Puyol.
0 comments :
Post a Comment