Mh Makinda ameyasema hayo alipokuwa akiongoza
mkutano wa kumi na nne na kikao cha kumi na tisa ambapo amesema
anashangazwa na maneno maneno ambayo wabunge wamekuwa wakitupiana
wakati anawajua wote waliochukua fedha bila ya kusafiri.
Katika hatua nyingine wabunge walipata nafasi ya
kumuuliza maswali ya moja kwa moja Mh Waziri Mkuu ambapo Mh Joshua
Nasari Mbunge wa Arumeru mashariki alitaka kujua kuhusu vitendo vya
raia kubamimbikizwa kesi na hasa tukio la kulipuliwa kwa bomu huko
Arusha kama ni nia ya .
Naye mh James Mbatia alimuliza mh pinda
serikali inamikakati gani kuhusu kukabiliana na msongamano wa
magari hasa katika jiji la Dar es salaam , ambapo waziri mkuu
akasema serikali ipo tayari kuunda timu ndogo ambayo
itamuhusisha mh mbatia ili kupata ufumbuzi wa tatizo hilo.
Kutokana na hatua hiyo ya kuundwa kwa timu
hiyo ndogo ya kupata ufumbuzi wa msongamano katika jiji la
Dar es saalam ITV ilimtafuta Mh Mbatia kwa lengo la kupata mawazo
yake ambayo anakusudia kuyafikisha katika timu hiyo itayoundwa
katika kupata ufumbuzi wa msongamano wa magari jijini Dar es
Salaam .
Ikiwa ni siku ya pili kwa wabunge kuchangia
katika taarifa ya kamati mbili za bunge zilizowasilisha taarifa
zake baaadhi ya wabunge wameendelea kuchangia taarifa hizo
huku Mh Rebeca Mndogo mbunge wa viti maalum kwa tiketi ya chama cha
demokrasiaa na maendeleo Chadema ameiomba serikali ihakishe
miradi mikubwa inafanywa na sekta binafsi.Source ITV
0 comments :
Post a Comment