.

.

SHOP HERE

News
Loading...

.

.

.

shop now

Kikosi kipya Yanga matata

 
UJIO wa straika, Emmanuel Okwi umetikisa kikosi cha kwanza cha Yanga na wachezaji kadhaa wanaelekea kupoteza nafasi zao na wengine wataendelea kuwekwa benchi.
Mchezaji wa kwanza anayekumbana na panga la kwenda benchi ni Hamis Kiiza ambaye hucheza nafasi za straika na wakati mwingine winga.
Uhusiano uliopo kati ya Kiiza na kocha, Ernest Brandts, si mzuri hasa baada ya kutorudi katika benchi la timu hiyo alipofanyiwa mabadiliko katika mchezo wa mwisho wa timu hiyo dhidi ya JKT Oljoro.
Kiiza ni mchezaji anayeenda benchi kukutana na Jerry Tegete ambaye alikuwa akisubiri makosa ya Kiiza au Didier Kavumbagu ili acheze, hiyo ina maana nafasi yake inazidi kuwa finyu kucheza kikosi cha kwanza.
Mshambuliaji atakayekuwa benchi akisubiri kuchukua nafasi ya Okwi au Kavumbagu atakuwa Kiiza ambaye awali alikuwa kikosi cha kwanza. Hapo Tegete anaweza kuwa chaguo la tatu kama atazembea mazoezini.
Kama Brandts ataamua kumtumia Okwi kama winga pale anapoona inafaa, ni wazi Haruna Niyonzima ataanzia benchi kwani nafasi yake katika kiungo ni finyu kwani wapo Frank Domayo, Hassan Dilunga na Athuman Idd ‘Chuji’. Domayo, Dilunga na Chuji mmoja wao lazima aende benchi ili wawili tu wacheze hivyo Niyonzima anahesabika kama winga anayecheza kwa kuingia ndani wakati mwingi.
Yanga imesajili wachezaji watatu tu katika dirisha dogo la usajili msimu huu wa Ligi Kuu Bara ambao kwa hali ilivyo na ufanisi wao wanaingia moja kwa moja katika kikosi cha kwanza.
Wachezaji hao ni kipa Juma Kaseja aliyesajiliwa akiwa mchezaji huru, kiungo Hassan Dilunga aliyetokea Ruvu Shooting na Okwi kutoka SC Villa ya Uganda.
Kikosi cha Yanga kinachoundwa na wachezaji wapya, kitawaweka benchi wachezaji watatu wa ‘First Eleven’ ya zamani ambao ni kipa Ali Mustapha ‘Barthez’, kiungo Chuji na mshambuliaji Kiiza.
Kikosi kipya cha kocha Brandts kitakuwa hivi;
Juma Kaseja (kipa), Mbuyu Twite na David Luhende (mabeki wa pembeni), Kelvin Yondani na Nadir Haroub ‘Cannavaro’ (mabeki wa kati), Frank Domayo, Hassan Dilunga na Haruna Niyonzima (viungo) pamoja na Mrisho Ngassa, Didier Kavumbagu na Emmnuel Okwi (washambualiaji).
Katika benchi watakuwepo Barthez, Oscar Joshua, Juma Abdul, Chuji, Kiiza, Jerry Tegete na Said Bahanuzi. Hata hivyo katika mechi za Yanga kunaweza kukawepo kwa mabadilishano wa nafasi kati ya Dilunga na Chuji.
Share on Google Plus

About feisal pinto

Computer Application Student, Author, Short Stories Writer, Business Proposal Writer, Presenter and Application Builder. Email feisalpinto4@gmail.com for complains and business only.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment

ad