Ni zile stori za town sasa hivi ambapo mwigizaji Kajala amezungumza kwa mara ya kwanza kuhusu ishu yake ya kuandikwa kwenye blogs na magazeti ya bongo kuhusu tuhuma za kuchukua mume wa mtu.
Kajala anasema picha iliyopigwa akiwa na huyo mume wa mtu, kwanza ilipigwa bila yeye kujua lakini pia anasisitiza kwenda club au kwenda sehemu na kukutana na mtu na kupiga nae picha sio kwamba ndio umemuiba.
Anasema siku ya tukio ilikua ni siku ya kuzaliwa kwa mmiliki wa club hii ndio ikawa party hivyo kila mtu alikua anapiga picha ovyo ovyo ndio maana hata yeye hakujua kama anapigwa.
Kajala ambae ni mama wa mtoto mmoja mwenye umri wa miaka 14, anasema picha hii na taarifa za kuiba mume wa mtu zimemletea tatizo na maswali kwa familia yake hasa Mtoto na Mama yake.
Anasema mama yake mzazi aliumwa kwa mshtuko alioupata kwa sababu alidhani mwanae kaenda China kikazi na sio kuchukua mume wa mtu.
0 comments :
Post a Comment