BEKI wa zamani wa Simba, Shomari Kapombe aliyekuwa anaichezea klabu ya As Cannes ya Ufaransa inayoshiriki Ligi Daraja la Nne juzi Jumapili aliongozana na Mrisho Ngassa mguu kwa mguu kuiona Azam FC ikicheza na Ferroviario ya Msumbiji.
Ingawa haijulikana walitokea, lakini Kapombe
anayewindwa na Yanga, aliingia kwenye Uwanja wa Azam Complex uliopo
Chamazi nje kidogo ya Dar es Salaam akiwa na Ngassa kuangalia pambano la
Kombe la Shirikisho Afrika baina ya Azam FC na Ferroviario.
Beki huyo mara baada ya kuingia uwanjani hapo,
walikaa jukwaani na kufuatilia mechi hiyo kwa makini iliyomalizika kwa
Azam FC kushinda bao 1-0 na baadaye wakaondoka pamoja.
Tofauti na hao, wachezaji wengine wa Yanga waliofika uwanjani hapo kwa ni Emmanuel Okwi, Hamis Kiiza na kipa Juma Kaseja .
Mara baada ya mechi hiyo kumalizika, Kapombe
aliongoza na kiungo huyo na kuondoka zao muda mfupi baada ya Okwi na
Kaseja kuondoka.
Kapombe yuko nchini baada ya kugoma kurudi Ufaransa akishinikiza kulipwa malimbiko ya mishahara na stahiki zake.
Habari za ndani zinasema kuwa Kapombe amekuwa
karibu na viongozi wa Yanga na kuna uhakika mkubwa msimu ujao anaweza
kuvaa jezi za njano na kijani.
0 comments :
Post a Comment