Luke Shipley na Tom Hunt ni wana mitindo wawili wakiingereza waliozindua aina mpya ya Nguo za Kiume zilizopewa jina la (Meggings ) ambazo zitawawezesha kuwa huru na kujisiskia wepesi pindi watakapo kua wamezivaa. Ni aina flani ya nguo ambayo imezoeleka kuvaliwa na jinsia ya kike, inajulikana kama Leggings. Walizindua rasmi aina hii ya nguo huko Uingereza baada ya wao kulazimishwa kuvaa aina hio kwenye mmoja ya Maonyesho ya Mavazi.
Aina hio ya nguo ya ambao ni kwa ajiri ya wanaume imekadiriwa kuuzwa kwa takribani £25, huku vazi hilo likiungwa mkono na watu maarufu kama Russel Brand na Justin Bieber.
"huu ni muda wa wanaume kuvaa wanachokitaka na kuwa huru, tumefikiria na tumeona kwamba kwa kufanya hivi itasaidia watu kujielewa na kuwa huru" waliandika kupitia mtandao wao.
0 comments :
Post a Comment