Baba wa Lupita Nyong'o amesema maneno hayo wiki kadha baada ya Lupita Nyong'o kupewa tuzo ya Oscar, Lupita ambae ni binti wa kikenya ambae alipewa tuzo hio kwa umahiri wake alioonesha kwenye movie ya 12 YEARS A SLAVE,
Baba wa Muigizaji huyo amejitokeza na kueleza jinsi gani familia yake ilivyoteseka na kunyanyaswa nchini kenya.
Huku Lupita akiwa anasifiwa na muongozaji wa Movie hio kuweza kuigiza vipande vyake vizuri mpaka kufikia hatua ya kupewa tuzo, uigizaji wake kwenye vipengele vya kusikitisha, ila familia yake pia walikua watu wakuteswa, kunyanyaswa na pia kuuliwa.
Baba yake Lupita Nyong'o Mr Peter Anyang Nyong'o akiwa na binti yake Lupita wakati wa tuzo za Oscars |
kama mpinzani wa aliekua Raisi wa Kenya Daniel Arap Moi, baba yake muigizaji huyo, Peter Anyang Nyong'o ambae ni mwanasiasa nchini Kenya alikuwa akiteswa mara kwa mara, huku mwili wa Mjomba yake Lupita aitwae Charles Nyong'o haujaonekana mara baada ya mjomba huyo kuvamiwa akiwa feri na kutupwa nje ya meli.
Lupita akifurahia mara baada ya kupewa tuzo hio ya Oscar |
Peter Nyong'o, sasa ni kiongozi mwanasiasa anaetumikia kwenye seneti ya nchi, ameeleza ukweli wa ndani walichokuwa wakifanyiwa, mpaka kuhamua kukimbilia nchini Mexico ambapo Lupita alizaliwa mwezi Machi 1983.
Mr Nyong'o alieleza jinsi alivyo sumbuka kumwangalia mtoto wake akifanikiwa kwenye uigizaji.'Tuliwekwa Jela, kwenye machemba ya mateso, ila ilkua kama sherehe ya chakula cha usiku ukilinganisha na walichopitia watumwa,' mr Nyong'o aliiambia mtandao wa
Independent On Sunday
mr Nyongo pia alisema kaka yake Charles alipotea mwaka 1980, miaka miwili baada ya Moi kuwa raisi, na ndo wakati Mr Nyong'o akiongolewa kama mgumu kwenye siasa.
Mwili wake haukupatikana na hakuna mtu aliepelekwa mbele ya haki kwa mauaji hayo.
'Hata sasa, hakuna maelezo yaliotolewa kuhusu mauaji hayo. ninachokijua alikua feri huko mombasa na shuhuda nilieweza kuongea nae alisema haikua ajari ila alivamiwa na kusukumwa kutoka kwenye meli. Ila mashuhuda walikua na uoga wa kueleza mbele ya polisi,' alisema Mr Nyong'o
Mr Nyong'o ana amini yakwamba kaka yake aliuliwa kutoka na upinzani wake na Mr Moi.
Wachunguzi wana amini kwamba Moi na watu wake walichukua hela za matumizi ya Kenyaa zaidi ya £3 billion katika miaka 24 yake ya Uongozi, na pia anajulika kwa jinsi alivyokuwa akitumia ulinzi wa nchi kuua na kutesa.
Mr Nyong'o na mke wake walilazimika kuondoka kenya na kwenda Mexico, alipopata kazi ya kuwa mwalimu wa Siasa ya kisayansi, na ndipo Lupita alipo zaliwa.
Familia yake ilirejea kenya 1987 ila walikua wakijificha kwenye nyumba za siri, kwa sababu mr Nyong'o alikua akitengeneza chama cha siasa chini chini.
Akiwa msichana mdogo Lupita pamoja na kaka na dada zake watano walitakiwa kusafiri na wazazi wao kila mahali, huku baba yao akiwa anachuliwa na polisi kila wiki, huku wanafamilia wengine wakiwa ni wakupigiwa simu za vitisho kila siku.
Mr Nyong;o ambae ni mwanasiasa nchini Kenye anaamini kwamba kaka yake aliuliwa kwasababu ya upinzani wake na Raisi wazamani wa kenya Mr Daniel Arp Moi (Pichani) |
Mr Nyong'o alifikia hatua ya kufikiri Lupita hayupo huru kwenye kukuza na kuzingatia malengo yake, kuweza kumudu makazi mapya ilimsaidia kugeuza malengo yake na kuwa muigizaji
Mr Nyong'o na Mke wake walisafiri kutoka Kenya kwenda kuhudhuria tuzo hizo za Oscar ambapo mtoto wake alichukua tuzo pia.
Alisema "Lupita alinipigia na kuniambia alipochaguliwa kuwania tuzo hio. Aliguswa sana kwa kuwa alifanya vizuri mpaka kuchaguliwa kuwania tuzo hio.
Moja ya Vipengere alivyo igiza Lupita Nyong'o kwenye Movie ya 12 YEAR A SLAVE ambayo ilimuwezesha kupata Ushindi wa Tuzo za Oscar |
Lupita Nyong'o |
0 comments :
Post a Comment