Katibu wa NEC Itikadi na
Uenezi Nape Nnauye akimnadi mgombea wa nafasi ya ubunge jimbo la
Chalinze kupitia CCM Ndugu Ridhiwani Kikwete kwenye mkutano wa kampeni
uliofanyika kwenye kijiji cha Mazizi ambapo alisema moja ya sifa za
mgombea ni kuwafahamu wananchi wake, na wananchi wake kumfahamu,
kufahamu changamoto za wananchi na kufahamu namna ya kuzitatua
changamoto hizo.
Ridhiwani Kikwete akijinadi
kwa wananchi wa kijiji cha Mazizi kata ya Msata ambapo aliahidi kujenga
shule,kusaidia wakina mama na vijana,kushirikiana na wana Chalinze
katika kutafuta ufumbuzi wa matatizo ya afya,kuinua kilimo,kufanya
juhudi za dhati kuboresha kilimo.
Mjumbe wa Mkutano Mkuu wa
CCM Taifa Ndugu Ridhiwani Kikwete akifungua shina la Tonga Road wakati
wa ziara za mikutano ya kampeni za ubunge.
Katibu wa NEC Itikadi na
Uenezi Nape Nnauye akihutubia wakazi wa kijiji cha Tonga wakati wa
kumnadi mgombea wa CCM jimbo la Chalinze Ndugu Ridhiwani Kikwete.
Wazee wa kijiji cha Diozile
wakisoma vipeperushi vyenye wasifu wa Ridhiwani Kikwete wakati wa
mkutano wa kampeni za ubunge jimbo la Chalinze zilizofanyika kwenye
viwanja vya shule ya msingi Lubaya.
Kila aina ya furaha kwa
vijana wa Msoga ambapo mgombea wa Ubunge jimbo la Chalinze Ndugu
Ridhiwani Kikwete alifanya mkutano wa hadhara kwa wananchi wa kijiji
hicho.
Karibu wa NEC Itikadi na
Uenezi akihutubia wapiga kura wa Ridhiwani Kikwete wakati wa mkutano wa
kampeni uliofanyika Msoga ambapo wananchi hao wamesema kijijini kwao
hakutokuwa na kura kwa wapinzani.
Mjumbe wa Mkutano Mkuu wa
CCM Taifa Ndugu Ridhiwani Kikwete akikata utepe kufungua shina la UVCCM
Msoga baada ya kumaliza mkutano wa hadhara wa kampeni za ubunge.








0 comments :
Post a Comment