Shabiki wa mmoja wa klabu ya Liverpool huko nchini Kosovo ameweka kiapo kilichodumu kwa miaka 11 juu ya klabu ya Liverpool.
Shabiki huyo aliyefahamika kwa jina la Ukë
Krasniqi aliweka kiapo cha kutokukata nywele zake miaka 11 – kuanzia
mwaka 2003 mpaka leo hii, akiapa kwamba hatozikata nywele hizo mpaka
pale Liverpool itakapotwaa ubingwa wa Uingereza maarufu kama Barclays
Premier League.
Hivi sasa story hiyo ya raia huyo wa Kosovo
imetengeneza headlines na gazeti la Kosovo Republika.mk, limemfanyia
mahojiano Ukë Krasniqi na haya ndio aliyosema:
“Tangu mwaka 2003 nilianza kufuga nywele zangu…Mpaka sasa
Liverpool imeshinda kila kombe lakini sio Premier League. Sasa
tumekaribia kushinda ubingwa huo. Hata kama tutangazwa mabingwa mapema, nitaendelea kufuga nywele zangu mpaka May 11. Nataka kushangilia na nywele zangu wakati Steve Gerrard atakapobeba kombe kwa mara ya kwanza, kisha baada ya hapo nitakata.”
0 comments :
Post a Comment