.

.

SHOP HERE

News
Loading...

.

.

.

shop now

BABU SEYA NA MWANAE WAACHIWA HURU, HII NDIO TAARIFA RASMI KUTOKA JESHI LA MAGEREZA




Na:Blog Ya Vijana

Kuna taarifa imekua zikienea kwenye mitandao ya kijamii na pia zingine kutumwa kupitia ujumbe mfupi wa message sms kwamba Babu seya na mwanae ambao wanatumikia kifungo cha maisha katika gereza la Magereza kwamba wameachiwa na wako huru, Jeshi la Magereza wamekanusha uzushi huo na kutuma ujumbe huu kwa wananchi wote 


TAARIFA RASMI KUTOKA JESHI LA MAGEREZA KUHUSU TAARIFA ZA UZUSHI ZINAZOZAGAA KUWA BABU SEYA NA MAWAE WAMEACHIWA HURU

Hivi sasa kuna taarifa zimesambaa kupitia Ujumbe mfupi wa simu (SMS) na mitandao ya kijamii zikihusisha kuachiliwa huru kwa wafungwa wa
wili wanaotumikia Kifungo cha Maisha gerezani. Wafungwa hao wanaotajwa ni Nguza Vicking(Maarufu kwa jina Babu Seya) na Johnson Nguza(Maarufu kwa jina la Papii Kocha).

Napenda kuufahamisha Umma wa Watanzania kuwa taarifa hizo zote zilizotolewa kupitia njia hizo ni za Uongo na uzushi mkubwa na zinalenga kuipotosha jamii kwani wafungwa hao wapo gerezani na wanaendelea kutumikia adhabu ya kifungo cha Maisha gerezani kwa mujibu wa Sheria.

Jeshi la Magereza nchini linatoa onyo kali kwa watu kujiepusha na uhalifu huo na linawataka wale wote wanaotumiwa ujumbe wa aina hiyo waepuke kuusambaza ujumbe huo kwa wengine bali waufute, kwani kuendelea kuusambaza ni kosa kisheria.

Aidha, Jeshi la Magereza linaendelea na uchunguzi wa kina ili kuwabaini wanaosambaza ujumbe huo likishirikiana na Vyombo vingine muhimu kwa lengo la kuwakamata wahalifu hao ili mkondo wa Sheria uchukue nafasi yake.

Imetolewa na;
Lucas Mboje, Mkaguzi wa Magereza,
Afisa Habari wa Jeshi la Magereza,
Makao Makuu ya Jeshi la Magereza,
DAR ES SALAAM.
Septemba 8, 2014



Huo ndo ujumbe waliotuma Jeshi la Magereza kuhusu uzushi huo, kama unalolote la kusema basi acha comment yako chini ya habari hii .......
Share on Google Plus

About feisal pinto

Computer Application Student, Author, Short Stories Writer, Business Proposal Writer, Presenter and Application Builder. Email feisalpinto4@gmail.com for complains and business only.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment

ad