Mtengenezaji wa filamu mkongwe hapa nchini, William Mtitu ameendela kuwaponda baadhi ya wasanii ambao wanafanya kazi na kampuni ya Steps Entertainment kwa kukubali kushisha bei ya kazi zao kutoka shilingi 3000/= hadi shilingi 1,500 /= kwa CD moja kwa rejareja.
Kupitia ukurasa wake wa INSTAGRAM, Mtitu aliweka picha hiyo hapo juu na kuandika maneno haya;
"Wakati tukiangaika maporini kushuti sinema zenye ubora wasanii wenzetu sijui tuite upumbavu au kutojielewa wanajifungia ndani na wàhindi wao wawili eti wanataka kushusha bei sinema bei ya jumla iwe ziuzwe elfu moja (1,000/=)na rejàreja ziuzwe elfu moja na mia tano(1,500/=) hii nizi ni njama ili kuua wasambazaji wengine na ni dharau kubwa sana kwa wale wote waliotoa nguvu zao kwa hali na mali mpaka tasnia ya sinema imefika hapa ilipo,
kiukweli atuwezi kukubali hata kidogo na lazima tushinde hivi vita kwa gharama yeyote".
Siku kampuni ya Steps Entertainment ilipotangaza swala hili la ushushwaji wa bei za filamu Mtitu aliweka picha hii ya baadhi ya wasanii wakiwa kwenye mkutano na wandishi wa habari na kuandika haya:
"Ama kwa hakika hawa wahindi(steps entertainments wameamua kutumia wasanii wenzetu kutaka kutua kibiashara baada ya kuona sasa tumeamua kujikomboa sisi wasanii wa filamu kwa kuamua kusambaza sinema zetu wenyewe baada ya kuwatajilisha kwa muda mrefu nyinyi wenyewe mashahidi marehemu kanumba na sajuki wamekufa maskini hali hawa wahindi wanapata mamilioni
kutokana na kazi zao mpaka leo,angalia kàtika hiyo picha hao wote ni wasanii wenzetu wanamsaidia adui ili atumalize da hii inauma sana watanzania wenzangu .lakini nawahakikishi hivi vita lazima tutashinda kwa gharama yeyote maana haya ni maisha yetu kwani wale wahindi biashara ya sinema ikifa watauza sora ,toyo au wataendelea na biashara ya hotel yao ya sunrise narudia tena hivi vita lazima tutashindi kwa gharama yeyote".
Una maoni gani juu ya hili
0 comments :
Post a Comment