.

.

SHOP HERE

News
Loading...

.

.

.

shop now

Maneno ya DUDE kwenda kwa Q-Chillah “Namkumbusha Q-Chillah huku kugumu kuliko kwenye..."

Dude Ampa Makavu Q-Chillah
MWONGOZAJI na mwigizaji mkongwe katika tasnia ya filamu Swahilihood, Kulwa Kikumba ‘Dude’ amemtolea uvivu msanii wa muziki wa kizazi kipya na mwigizaji wa filamu, Shabani Katwila ‘Q-Chillah’ kwa kumwambia kuwa katika filamu hakuna ubishoo zaidi ya uhalisia na uhusika kwa filamu husika.
“Napenda kumwambia mdogo wangu Q-Chillah huku siyo kama katika muziki, huku tunavaa kulinga na uhusika, siyo kuvaa tu ilimradi umevaa tu, maskini hawezi kuvaa suti, au mchungaji kuvaa pensi au kuonekana tofauti na hadithi inavyosema.
“Namkumbusha Q-Chillah huku kugumu kuliko kwenye muziki anakotaka na tunavaa kulinga na uhusika hakuna ubishoo,” alisema.
Dude alisema hayo kufuatia kauli ya Q- Chillah kuwa wasanii wengi wa filamu hawajipangi katika mavazi, wakati yeye anapoingia katika filamu yoyote anajipanga na kununua nguo za kutosha hadi kutumia milioni kwa ajili ya filamu anayoigiza.
Share on Google Plus

About feisal pinto

Computer Application Student, Author, Short Stories Writer, Business Proposal Writer, Presenter and Application Builder. Email feisalpinto4@gmail.com for complains and business only.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment

ad