.

.

SHOP HERE

News
Loading...

.

.

.

shop now

VINCENT KIGOSI ANENA "..kuna watu ambao nikiwa nao hujifanya kunisifia nikiwapa kisogo tu huni..."

VINCENT Kigosi ‘Ray’ amesema kuna baadhi ya watu wakiwamo wasanii, huwa wanawadharau wakongwe walioifanya tasnia hiyo kuwa juu na kuwasema vibaya pindi wanapowapa kisogo.
Ray alisema kuwa baadhi ya wasanii wachanga leo hii wanauza kazi zao na kukaa na wakongwe na kuwasifia lakini wakiwapa kisogo wanawasema vibaya.
“Tasnia hii watu waliisusa ilikuwa ikionekana kama ni kazi ya ziada tu wala si kazi inayomwezesha mtu kuendesha maisha yake, katika hali ngumu tulipigana na kuifikisha hapa, wasanii wakongwe ndio tuliopigania, leo wanatubeza kwa sababu wanauza filamu zao,” alisema Ray.
Ray alisema hivi sasa tasnia inatolewa macho na kila mtu kuwa ni ajira kwa watu hata serikali imeliona hilo. Ray alisema ili kuhakikisha kazi zake zinakuwa bora kila mara hutumia muda mwingi kuongeza vifaa vya kisasa sambamba na kutumia watu wenye ujuzi wa filamu.
“Lakini bado najua kuna watu ambao nikiwa nao hujifanya kunisifia nikiwapa kisogo tu huniponda,” alisisitiza.
Ray anashauri vijana washindane katika kazi na si kupoteza muda kwa kuwabeza watu na kuzungumzia majungu.
Share on Google Plus

About feisal pinto

Computer Application Student, Author, Short Stories Writer, Business Proposal Writer, Presenter and Application Builder. Email feisalpinto4@gmail.com for complains and business only.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment

ad