.

.

SHOP HERE

News
Loading...

.

.

.

shop now

Kajala: "Najua siku Moja tutaishia kama Zamani." aeleza mengi juu ya Wema Sepetu na Petit-Man

Kupitia ukurasa wa mtandao wa kijamaa instagram wa muigizaji wa filamu za kitanzania, Kajala Masanja ameandika ujumbe wa mzito ulioambatana na picha ya Wema Sepetu pamoja na Petit-Man.

Ni muda sasa tangu Wema na Kajala kuingia katika ugomvi wa mambo yao binafsi mpaka kupelekea pande zote mbili za mashabiki wao kuendeleza na kuchochea mtafaruku huo.

Katika ujumbe huo ambao ndani yake kuna hisia za upole na mifano tofauti na mengine mengi.

Soma Ujumbe huo mzito hapa chini...


BINADAMU TULIUMBWA KUISHI KATIKA MISINGI YA UBINADAMU NA SIO 
UNYAMA KAMA WAISHIVYO WANYAMA WA PORINI LEO NAOMBA KUSEMA 
KUTOKA MOYONI MWANGU.. NAJUA KABISA NINA WAZAZI WANGU NDUGU ZANGU NA ZAIDI SANA MUNGU WANGU ILA KUNA WATU MPAKA NAKUFA KAMWE SINTOWASAHAU KATIKA KUTA ZA MOYO WANGU KATIKA KIPINDI CHANGU KIGUMU NILICHOPITIA MLIKUWA NEMBO NAMBONI KUBWA KATIKA KUOKOA MAISHA YANGU... NAPENDA KUSEMA KUWA HATA KWA HAYA YOTE TUNAYOPITIA BADO NI MADOGO SANA KUFICHA THAMANI YENU MLIYOIJENGA JUU YANGU..NAKUMBUKA SANA MLIPOJITOA KWA AJILI YANGU MLIPOJINYIMA KWA AJILI YANGU MLIPOPIGANA KWA AJILI YANGU,MLIVYOFEDHEHEKA KWA AJILI YANGU YOTE HAYO NAYAKUMBUKA NA NAMSHUKURUU MUNGU KWANI NAONA KABISA MLILETWA DUNIANI KWA SABABU NYINGI NA MOJA YA SABABU ILIKUWA KUNIOKOA KATIKA KIPINDI KIGUMU KATIKA MAISHA YANGU.LEO HII TAREHE 25.5.2015 NAPENDA KUSEMA KWA UMMA NA ZAIDI KWA MUNGU WANGU KUWA NAWATHAMINI NAWAPENDA NA NASHUKURUUU SANA KWA YOTE MLIYOFANYA JUU YANGU.. NAWAOMBEA KWA MUNGU MUENDELEE NA MOYO HUO HUO KWANI NAAMINI KUNA WENGI BADO WANAWATEGEMEA ILI KUKOMBOA MAISHA YAO KWA WAKATI ALIYOPANGA MUNGU HATA KITABU CHA DINI KILISEMA KUWA "huwezi kumpenda Mungu usiyemuona wakati unamchukia ndugu yako unayemuona" NAJUA SIKU MOJA TUTAISHI KAMA ZAMANI.. AHSANTENI.



Ntajie list ya Mastaa ambao hawapo katika maelewano na ungependa waige mfano wa Kajala.....
Share on Google Plus

About feisal pinto

Computer Application Student, Author, Short Stories Writer, Business Proposal Writer, Presenter and Application Builder. Email feisalpinto4@gmail.com for complains and business only.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment

ad