MKONGWE wa muziki wa kizazi kipya nchini, Juma Kassim 'Sir Nature', ameahidi kujenga msikiti pamoja na madrasa ya watoto ikiwa ni kujenga na kukuza msingi na imani ya dini ya kiislamu.
Hayo yalisemwa na Nature mwishoni mwa wiki Dar es Salaam, wakati akifuturisha watu nyumbani kwake na kusema anafikiria mambo mengi kuyafanya katika jamii yake lakini tatizo kubwa ni fedha za kutosha kwani kila kitu kinahitaki fedha kutumika.
Alisema ana imani kuwa Mungu, ana makusudi yake na kudai kuwa ameshaweka nadhiri kwa Mungu kuwa amjalie fedha ambayo itamsaidia kutimiza azma yake kama ambavyo amemjalia kupata fedha kidogo ya kuweza kufuturisha watu.
Alisema kila kitu kinapangwa na Mungu kwa makusudi na angekuwa na fedha kama wanaoenda Afrika Kusini, kula bata kwa sifa angeweza kutimiza azma yake haraka.
0 comments :
Post a Comment