.

.

SHOP HERE

News
Loading...

.

.

.

shop now

Wema Sepetu na Lulu Michael wapigiwa debe Hollywood



Kama kweli wamedhamiria kufanya vizuri, huenda wasanii hawa Wema Sepetu na Elizabeth Michael 'Lulu' wakafika mbali katika fani hii ya uigizaji ambayo imechangia kuwapa umaarufu nchini.

Inaelezwa kuwa wana uwezo kufanya vizuri na vya kutisha hata wakiwa Hollywood, ikiwa wakipewa mwongozo mzuri.

Mwandishi, mtengenezaji na muigizaji wa filamu mpya ya 'Going Bongo', Ernest Nepoleon, amesema wawili hao ni noma na wanaweza kukamua hata kwenye anga za juu za filamu ikiwamo Hollywood.

"Kwa ujumla ni kwamba Tanzania tuna waigizaji wengi wazuri, watu wakiangalia Bongo Movie wanaona movie mbovu, hilo siyo suala la uigizaji, hayo yanakuwa ni mambo mengine ya utayarishaji yanayofanya filamu iwe mbovu," alisema.


"Wema na Lulu, kama wasanii wanaweza kufanya vizuri wakielekezwa mambo ya msingi. Lulu ni kama muigizaji wa Marekani, Lindsay Lohan, wote walianza kuigiza wakiwa na umri mdogo," alisema zaidi msanii huyo.


Akimzungumzia Wema Sepetu, Nepoleon alisema kuwa tayari ana kipaji cha kupendwa na watu wengi na wanajua ana kipaji kama Obama ambaye kila akiongea tu wanamsikiliza.

"Mtu kama Wema ana kipaji, ukiunganisha na uwezo wake wa kuigiza na akawekwa kwenye mradi ambao unamfaa, anaweza kufanya makubwa wanavyofanya wasanii wa Hollywood," alisema.
Share on Google Plus

About feisal pinto

Computer Application Student, Author, Short Stories Writer, Business Proposal Writer, Presenter and Application Builder. Email feisalpinto4@gmail.com for complains and business only.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment

ad