Hospitali ya African Medical Inverstment Ltd (AMI) maaarufu kama Trauma Center ya Msasani jijini Dar es salaam imefungwa baada ya kushindwa kulipa kodi ya pango kwa zaidi ya miezi 26.
hatua hii imefikiwa baada ya mabishano ya muda mrefu ya kisheria baina ya AMI inayodaiwa zaidi ya dola millioni 1.6 (sh. Billioni Tatu) na mfanyabiashara ambaye pia ni mmiliki wa jengo hilo, Navtej Sing Bains."
Akaunti za hospitali hiyo katika Benki ya Exim zilizoambatanishwa na Mahakama zimekutwa zimefungwa na fedha zote zikiwa zimetolewa.
Amri hiyo iliotolewa Alhamisi wiki iliyopita na kusainiwa na Makamu Msajili wa Mahakama kuu ya Tanzania, imeipa mamlaka kampuni ya mnada ya MEM (MEM Auctioneer's and General Brokers Limited) kuifukuza hospitali hiyo kwenye jengo hilo.
Amri hiyo itaanza baada ya kuisha kwa kipindi cha notsi cha siku 14 ambacho kimeshatumiwa na AMI. Amri hiyo sasa inachangia kufungwa kwa hospitali hiyo, licha ya rufaa zake kujaribu kuzuia kufukuzwa, baa da ya hospitali hiyo kushindwa kutimiza amri ya Mahakama ya Rufaa ya Tanzania ilioamuru kulipwa kwa dola milioni 1.514 za Marekani pamoja na kodi kila mwezi ya dola 64,000 kutokana na mgogoro wa kodi ya jengo. Jopo la majaji watatu wa Mahakama ya Rufaa, Mbarouk Mbarouk, Salum Massati na Katherine Oriyo waliamuru Hospitali ya AMI kufanya malipo hayo ndani ya Mwezi mmoja baada ya hukumu iliotolewa Februari 12, mwaka 2015, agizo ambalo halijatekelezwa.
0 comments :
Post a Comment