.

.

SHOP HERE

News
Loading...

.

.

.

shop now

Mtangazaji Maulid Kitenge aandika Barua ya Wazi kwenda kwa raisi mstaafu Alhaj Ally Hasan Mwinyi


Mchambuzi/Mtangazaji maarufu wa maswala ya Michezo nchini Tanzania, Maulid Kitenge (kulia) amemuandikia barua ya wazi raisi mstaafu Alhaj Ally Hassan Mwinyi kumuomba kutengua kauli yake aliosema Tanzania ni kichwa cha mwendawazimu.

Mtangazaji wa Sports Headquarter ya Efm (93.7 Dar es salaam), amemuandikia barua ya wazi raisi mstaafu mapema leo asubuhi katika kurasa zake za mitandao ya kijamii za facebook na Instagram kufatia kipigo cha Taifa stars katika mechi dhidi ya Swaziland iliochezwa jana {Tanzania 0 - 1 Swaziland}.(shuka chini kusoma barua hio)

Soma barua ya wazi kwenda kwa Raisi Mstaafu  Alhaj Ally Hasan Mwinyi

Kutoka kwa Maulid Kitenge

"BARUA YA WAZI KWA ALLY HASAN MWINYI. ==================================== AWALI YA YOTE KWANZA KABISA NAPENDA KUKUPA HESHIMA YAKO MZEE WANGU , RAIS WANGU MSTAAFU ALHAJ ALLY HASAN MWINYI SHIKAMOO MZEE. NIA NA DHUMUNI YA BARUA HII NI KUKUTAKA WEWE UKIWA KAMA MZEE WETU KUTENGUA KAULI YAKO ILEEE ULIYOSEMA TANZANIA NI KICHWA CHA MWENDAWAZIMU. KUMBUKA MZEE WANGU MANENO YA MTU MZIMA YAKITOKA HUWA HAYARUDI MATUPU . VIJANA WAKO TUNATAABIKA NA KAULI YAKO KWA MAANA MPAKA LEO INATUTAFUNA. ALHAJI MWINYI TUNAKUOMBA KWA MOYO MKUNJUFU TENGUA KAULI YAKO YA KUWA TANZANIA NI KICHWA CHA MWENDAWAZIMU ILI KULINUSURU TAIFA KATIKA MASWALA YA MICHEZO HUSUSANI MPIRA WA MIGUU. MZEE WETU HIVI SASA TUPO KATIKA HALI MBAYA KULIKO VILE KABLA HUJATOA KAULI YAKO KWA MAANA HAPO MWANZO TULIKUWA TUNAJIKONGOJA YANI UAFADHALI ULIKUWEPO. ZAMANI TIMU ILIKUWA HAINA MAANDALIZI MAZURI KAMBI ILIKUWA INAWEKA JESHI LA WOKOVU , WACHEZAJI WANAENDA MAZOEZINI NA DALADALA HUKU POSHO KUKIWA HAKUNA ILA WALIPIGANA NA KUILETEA NCHI HESHIMA. MHESHIMIWA TANGU UTOE KAULI YAKO ILE TAIFA STARS IMEKUWA KWELI KICHWA CHA MWENDAWAZIMU. HAKUNA WA KUINUSURU TAIFA STARS ZAIDI YAKO WEWE ALHAJ ALLY HASANI MWINYI. ONA LEO HII TUNAFUNGWA NA NCHI AMBAYO MFALME WAKE HANA ANACHOWAZA ZAIDI YA KUOA VIGORI KILA MSIMU UFIKAPO. MZEE WETU TUNAKUOMBA TENA NA TENA YANI TUPO CHINI YA MIGUU YAKO TENGUA KAULI YAKO ILI KUINUSURU STARS YETU. SINA MENGI ZAIDI MZEE WANGU ILA NATUMAI UJUMBE WANGU UTAKUFIKIA NA UTAUFANYIA KAZI. WAKO KATIKA UJENZI WA TAIFA."


Mapema hapo jana Kitenge alionekana mwenye huzuni na mshangao mkubwa baada ya kuandika maneno machache kufatia uzembe uliofanyika mpaka Swaziland kujipatia goli 1 la ushindi.



Baadhi ya folllowers wake wa instagram walikuwa na haya yakusema...!

george.hazardNdooo timu yetu tutafanyaje sasa

mnanaabouTimu haileweki inacheza mfumo gani. Msuva na boko ni uozo mtupu. Sijaona sababu ya kumchezesha nyoni namba 6 wakati una kazimoto na ndemla ndani ya timu. All in all tatizo kubwa ni kukariri kikoso

kimbiratim ya taifa bado sana tungewaiga kama senegal walijiondoa kwenye mshindano wakatengeneza timu hiliyofika robo fainal kombe la dunia na kumfunga mfaransa lkn kwa kocha huyu na timu hii daima tusahau furaha ndani ya mioyo yetu kwanza kocha ajui kufanya sub pili wachezaji hawajitambui.Bora KIM Paulsen Timu ilikuwa inaeleweka.MM BINAFSI SIPENDI FALSAFA YA KOCHA NOOJ IMEFIKIA WAKATI TUWAAMINI MAKOCHA WAZAWA WAPEWE TIMU N MASLAHI MAZURI TUTAFANYA POA.KHALIFA MZEE WA BUNJU

antonkamanda.akKaka kitenge amakweli stars kuiangalia unahitaji uwe na panado mufukoni lakini sitochoka kuishangilia anthony andrea wa mwananyamala mchangani

listerchimya2hamna timu kaka na huyo kocha ndo kichaa anazalilisha Taifa letu


Share on Google Plus

About feisal pinto

Computer Application Student, Author, Short Stories Writer, Business Proposal Writer, Presenter and Application Builder. Email feisalpinto4@gmail.com for complains and business only.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment

ad