Taarifa zilieleza kwamba star wa Real Madrid ametoa kiasi kikubwa cha pesa kwenda kwenye mfuko wa waliokubwa na tetemeko la ardhi.
Charity ya 'Save the Children' imekanusha taarifa kwamba Cristiano Ronaldo ametoa paundi millioni 7 kwenda kwenye mfuko wa waliokumbwa na tetemeko la Ardhi huko Nepal.
ilisemekana kwamba mchezaji huyo mwenye miaka 30 ametoa kiasi hicho cha pesa kwa taasisi kwa lengo la kusaidia Jitihada za uokozi nchini, na wawakilishi saba.
Taarifa kutoka mtandao wa charity ya 'Save the Children' walisema: " Balozi wa kimataifa wa Save the Children , Cristiano Ronaldo , ametumia sauti yake ili kuongeza uelewa wa matatizo yanayowakabili watoto wanaoishi katika mazingira magumu zaidi duniani."
"Lakini taarifa za hivi karibuni kuhusu mchango kutoka kwa Ronaldo kwa dharura ya Save the Children nchini Nepal ni uongo."
"Baada ya tetemeko la pili , ambayo imeleta uharibifu zaidi kwa nchi, taasisi isiyokuwa ya kiserikali inataka kuwashukuru Cristiano Ronaldo na watu wengine mashuhuri kwa msaada wao katika kutangaza hali inayowakabili watoto na familia huku Nepal."
Watu wanaokadiriwa 8,000 waliuawa wakati tetemeko kubwa lililo gonga nchi mnamo Aprili 25, kabla ya tetemeko la pili kupiga Mei 12, na kuua watu 16 zaidi.
Source: Goal.com
0 comments :
Post a Comment