Usiku wa Ijumaa (22/5/2015) story mitandaoni na kila sehemu ilikuwa kuhusu Tuzo za Watu 2015 (shukrani kwa bongo5 Media) kuandaa Tuzo ambazo zinafanyika kwa mara ya 2 tangu zianze mwaka 2014.
Ukiongelea Washindi wa Tuzo za Watu basi ni asilimia 100 wamepata tutokana na kura za watu, Tuliweza kushuhudia washindi wa 2015.
Nimekuletea list ya mastaa wakiume waliofika katika usiku huo wakiwa wamependeza,
(Bofya Hapa kuona mastaa ambao hawa kuvaa on Point)
(Bofya hapa kuona mastaa wakike waliopendeza) pale Hyatt Hotel jijini Dar es salaam.
- 1 Millard Ayo
Mtangazaji wa Clouds Media, Millard Ayo huwa hakosei kwenye mavazi pengine ni kutokana na washauri wa mavazi anao watumia, Usiku wa Tuzo za Watu mwaka 2014 alikuwa yupo classic na pia ametokea tena kwenye list ya 2015 ndani ya vazi la suit.
Ukiachana yeye kuwa 1 kwenye list bali pia amevalishwa na wabunifu wawili wa mavazi kutoka nchini Tanzania, Suit kutoka kwa Mbunifu, Sheria Ngowi na kiatu kutoka kwa mbunifu, Martin Kadinda (Mugatti Shoe). Super Millard Ayo.
- 2 Martin Kadinda
Manager wa 'Wema Sepetu' na Mbunifu wa mavazi maarufu nchini, Martin Kadinda alikuwa very super, cheki tie style "inaitwa Knot Bow Tie." aieleza Martin.
Sio ajabu sana kumuona Martin katika list kwani ni miongoni mwa fashion Designers anaeongoza kuweka trend ya ubunifu wake. Salute to him. Outfit ilikuwa nice touch.
- 3 Ommy Dimpoz
Mwanamuziki anaetamba na nyimbo ya Wanjera kwa sasa, Ommy Dimpoz jana alipiga suit moja Classic kutoka @jm_international_collection (instagram username) japo rangi yake tushaizoea sana ila alikuwa On Point as always.
- 4 Perfect Crispin
Mtangazaji wa Clouds Media, Perfect Crispin alikuwa on point katika usiku wa tuzo za watu, Ndani ya Single Button kisha Bow Tie ni amependeza sana. #OnPoint
- 5 Salim Kikeke
Mtangazaji wa Dira ya Dunia, Idhaa ya Kiswahili Duniani BBC Swahili, Salim Kikeke ambae pia jana aliondoka na Tuzo ya Mtangazaji wa Television anaependwa. Hio 'Bow Tie' perfect kabisa, Suit On poin.
- 6 Albert Msando
Mwanasheria wa Zitto Kabwe pia mshauri wa baadhi ya wasanii wakubwa nchini, Albert Msando alipendeza sana, ni kawaida kwa Albert kuvaa suit akiwa kazini kama mwanasheria, ila kwa usiku wa jana alikuwa na kila sababu ya kuwa kwenye List.
- 7 Jacob Stephen (JB)
Muigizaji wa movie za kibongo, Jacob Stephen alipendeza sana, na kuonekana mwenye furaha. Suit Coat ilimpendeza, pia aliweza kupangalia.. salute to Jb nampa 7
- 8 Petit-Man
Mtu wa karibu wa muigizaji wema sepetu pia Meneja wa mwana-muziki Mirror Mirror kutoka Endless Fame, Petit-Man jana alikuwa simple but classic, Salute kwa Mke wake 'Esma Platnum' kwa kumpendezesha katika usiku wa tuzo za watu 2015.
- 9 Josh Murunga
Mtayarishaji wa kipindi cha Mkasi, Josh Murunga alivaa full black, yani simple ila classic, Mwaka 2014 Josh alikuwa on point na ameendelea kuwa on point this year. Anafunga List katika nafasi ya 9
Niandikie List yako Ungempa nani 1 - 9...?
kusoma List ya Mastaa wakike waliopendeza BOFYA HAPA
Kusoma list ya Mastaa wakiume waliovaa Off-Point BOFYA HAPA
0 comments :
Post a Comment